Posts

Showing posts from July, 2008

UFAFANUZI KUHUSU MAMLAKA YA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA IBARA YA 30(5) YA KATIBA YA TANZANIA

MJADALA KUHUSU IBARA YA 30(5) YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977 . UTANGULIZI . Ndugu Wadau, Hivi karibuni kulibuka mjadala mkali sana kuhusu ibara ya 30(5) ya katiba ya Tanzania,mjadala ambao uliiibuliwa na Mwanakijiji akitaka kujua mambo yafuatayo:- 1. Je,mahakama ikisema sheria Fulani ni batili na kinyume cha katiba kwa mujibu wa ibara ya 30(5) sheria hiyo inatenguka mara moja? 2. Je, neno “badala” linapotumika katika ibara tajwa hapo juu ni sawa au neon baada ndilo lingetumika? 3. Kama mahakama inasema sheria Fulani ni kinyume cha katiba ni kwa msingi gani sheria hiyo inaendelea kutumika? Watu mbalimbali walichangai mada hii,kiasi cha kupelekea kuibua hoja au maswali mengine mengi (ambayo kisheria nayaita issues) yaliyohusiana na ibara hiyo.Moja ya maswali hayo ni kma yafuatayo:- 1. Je,nini kitatokea iwapo mahakama imeipa serikali muda wa maalumu mathalani miezi 3 kurekebisha sheria na serikali haikufanya hivyo,ipi ni hadhi(status) ya hiyo sheria au kip