NUKUU MUHIMU YA LEO

UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA.
Katika kitabu hicho Nyerere alianza kuwatahadharisha viongozi walioko madarakani kwa maneno haya “ Kimya kimya msidhani ni ishara ya amani.” Kwa maneno hayo Mwalimu Nyerere aliwaonyesha viongozi kuwa Watanzania wanaonekana wakimya, lakini siku moja wanaweza kuvunja ukimya kama watachoka na uongozi mbovu.
Ndiyo maana Mwalimu akakemea hoja ya utanganyika ambayo ilionekana kupitishwa na viongozi bila ridhaa ya wananchi. Hayati Nyerere aliona hatari ya kuwa na Serikali tatu ambazo alisema zingezaa Watanganyika, Wapemba na Wazanzibar.
Akasema umoja ungeondoka na amani ingetoweka. Ndipo akasema CCM ilishaingiliwa na kansa ambayo ilihitaji kushughulikiwa. Katika kitabu chake cha Uongozi na hatima ya Tanzania aliandika “

ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe vyama vya
upinzani.” anaendelea “Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri
ambacho kingeweza kuongoza nchi yetu badala ya CCM au ambacho kingeilazimisha
CCM kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa
katika uchaguzi ujao,”
Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia
yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa vyama
vya upinzani, kinaweza kuendelea kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya
uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua
chama chochote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi
kuyasema haya, lakini uhai wa nchi yetu unataka yasemwe


Mwalimu aliionya CCM ina haja ya kujichunguza na kubadilika ndipo
alipohitimisha kitabu chake kwa utenzi. Ole wake Tanzania, Tusipo-isaidia,
niwezalo nimefanya, kushauri na kuonya. Wananchi wanasema kama Nyerere
angefufuka hivi sasa wangemweleza jinsi ambavyo baadhi ya vigogo wenye uchu wa
madaraka ambavyo wameanza kutoa rushwa ili waweze kushinda urais katika uchaguzi
wa Rais utakaofanyika mwakani, angekuwepo angekemea vikali.




KUHUSU MAJUKUMU YA RAIS.
Hatuwezi kujijengea utaratibu wowote ambao utazuia kabisa makosa yasifanyike, hata makosa makubwa; lakini tunatazamia kuwa yakifanyika, wanaohusika watawajibika.

Na katika makosa makubwa ya maadili na utendaji, mwenye jukumu la wazi wazi la
kuwadhibiti wahusika ni Rais. Mawaziri wake wanapofanya makosa makubwa, na
badala ya kujiuzulu waanze kufanya hila na kutafuta visingizio vya kutofanya
hivyo. Ni kazi yake rais mwenyewe, asiyoweza kusaidiwa na mtu mwingine. Mtu
anaweza kumsaidia rais kumnong'oneza waziri wake kujiuzulu; lakini hawezi
kumsaidia kumfukuza waziri wake. Hiyo ni kazi ya rais peke yake. Asipoifanya,
kosa ni lake peke yake
Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa maslahi ya wenyewe, watatokea
watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi. Lakini
uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na inzi


AHADI ZA RAIS
-Orodha ya wala rushwa ninayo....-Orodha ya wauza unga ninayo....-Orodha ya majambazi ninayo.....

HOJA YA LEO: je,leo hii haya yanatekelezwa?

Comments

Popular posts from this blog

PASSING OF PROPERTY IN THE GOODS

SYSTEMIC RISK

PASSING OF PROPERTY IN THE GOODS